Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi ndio timu 6 tutakazoziona VPL msimu wa 2018/2019

2673 Premierleague1912ab 660x400

Wed, 7 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 itaanza rasmi kushirikisha timu 20 katika Ligi kama ilivyo kwa Ligi Kubwa duniani za LaLiga ya Hispania na Ligi Kuu England EPL, hivyo msimu huu ndio mwisho VPL kushirikisha timu 16.

Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania bara inashirikisha timu 16 lakini baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kuongeza idadi ya timu, kuanzia msimu ujao Ligi Kuu itakuwa na timu 20, hivyo msimu huu ukiisha zitashuka timu mbili na kupata 6 ambazo zitakamilisha idadi ya timu 20.

Leo February 5 2018 zimejulikana rasmi idadi ya timu zitakazopanda Ligi Kuu msimu ujao wa 2018/2019, timu zilizopanda Ligi Kuu msimu ujao ni Alliance ya Mwanza, African Lyon ya DSM, Biashara ya Mara, JKT Tanzania ya DSM, Coastal Union ya Tanga na KMC ya Kinondoni.

Matokeo ya game za Ligi daraja la kwanza

  • Kiluvya United 0-1 African Lyon
  • Friends Rangers 3-1 Mvumvumwa
  • JKT Tanzania 3-0 Mshikamano
  • Ashanti United 3-2 Mgambo JKT
VIDEO: John Bocco na Mzamiru Yassin walivyoifungia Simba leo vs Ruvu Shooting

Chanzo: millardayo.com