Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hitimana Thierry amtabiria makubwa Pablo Franco

HITIMANA THIERRY 1 Hitimana Thierry amtabiria makubwa Pablo Franco

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa muda wa klabu ya Simba, Hitimana Thierry ametoa neno kuhusu ujio wa kocha mpya wa klabu hiyo, Mhispania Pablo Franco na kusema ana imani kocha huyo ataivusha Simba kwenye kipindi kigumu kinachoipitia hivi sasa.

Hitimana amesema, “Nimefurahi kukutana naye naamini huu ni wakati wa kumpa muda na ushirikiano ili aweze kuitoa Simba mahala ilipo na kuipeleka mbele zaidi kama alivyofanya mtangulizi wake”. 

Hitimana ameyasema hayo kocha mpya wa Simba, Pablo Franco alipowasili nchini Novemba 10, 2021 na kutembelea kambi ya wachezaji na Uongozi wa klabu hiyo maeneo ya Bunju pembeni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam.

Chanzo: eatv.tv