Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hitimana Ataja Sababu Tatu Simba Kuteseka

HITIMANA Hitimana Ataja Sababu Tatu Simba Kuteseka

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

KOCHA Mkuu wa Simba, Raia wa Rwanda, Thierry Hitimana amefunguka mambo matatu yanayosababisha
washindwe kufanya vizuri tangu kuanza kwa msimu huu.


Hitimana amefichua mambo hayo kufuatia Simba kucheza mechi nne katika Ligi Kuu Bara ambapo imefanikiwa
kushinda mechi mbili na kutoka sare mechi mbili huku ikiwa ya katika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi
kuu ikiwa pointi nane.


Leo Jumatano, Simba inatarajia kucheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo katika mchezo
ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.


Akizungumza na Championi Jumatano, Hitimana alisema kuwa, wanapitia wakati mgumu kwa sasa kutokana na timu yao kukwamishwa na uwepo wa mambo matatu ambayo hayakuwepo katika msimu uliopita hali iliyopelekea kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi Kuu.












“Tuna mambo matatu ambayo tunapitia lakini jambo la kwanza presha imekuwa kubwa ingawa ni kawaida katika soka lakini kwetu imekuwa kubwa kwa sababu tumekuwa na matokeo mabaya ambayo mashabiki wa Simba Hitimana Simba ataja… walikuwa hawajayazoea maana msimu uliopita timu ilikuwa juu sana.


“Lakini kukosekana kwa wachezaji kama Clatous Chama na Luis Miquissone wao walisaidia kwa sehemu
kubwa Simba kufanya vizuri ukiangalia kwa nafasi ambazo wanacheza, Chama atacheza kumi na Miquissone 11 ambao walisaidia ila sasa wengi bado wapya hivyo shida ipo ambayo itakuwa ya mpito kwetu.


“Ukiangalia tuna wimbi kubwa la wachezaji ambao wapo majeruhi, mtu kama Chris Mugalu hayupo, Lwanga
hayupo ambao hao wanaanza kwenye kikosi hali ambayo inatulazimu kuwatumia wachezaji wengi ambao wanakaa benchi na kuendelea kujipanga ili tufanye vizuri ikiwemo mechi yetu ya kesho (leo
Jumatano),” alisema Hitimana.
Chanzo: globalpublishers.co.tz