Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii hapa mikakati ya Yanga ndani ya CAF

KAGAME YANGA Hii hapa mikakati ya Yanga ndani ya CAF

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: ippmedia.com

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuingia kambini Agosti 15, mwaka huu baada ya wachezaji wapya kuungana na wengine katika kambi yao iliyopo Kigamboni na baadaye kwenda nchini Morocco ambapo kitaweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Kandoro alisema maamuzi hayo ya kutafuta mechi nyingi za kirafiki za ushindani ni baada ya kuona ratiba kuwa ngumu huku wakielekea kushiriki michuano ya kimataifa wakati ambao Ligi Kuu Tanzania Bara itakuwa haijaanza.

Alisema wamejipanga vizuri kutafuta mechi nyingi za ushindani za kirafiki ambazo zitasaidia timu yao kujiandaa na michuano ya kimataifa ambayo kwa muda mrefu hawajashiriki huku sasa wakitaka kufanya vizuri.

"Ni kweli tumeona ratiba ya Ligi Kuu kuanza Septemba 29, mwaka huu huku michuano ya kimataifa nayo inaanza mapema.

Tumeona hilo na sasa tayari tumeanza kutafuta timu za ushindani ambazo tutacheza mechi za kirafiki ikiwamo siku ya Wananchi, pia timu itaenda nje ya nchi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya," alisema Kandoro. Kuhusu usajili mpya, alisema:

"Tumejipanga vizuri, mashabiki wanatakiwa kutulia na viongozi tunaendelea na mchakato wa usajili wa wachezaji wapya na wengine tunaona wanaendelea katika michuano ya Kagame na kufanya vizuri akiwamo Jimmy Ukonde.

Naye Ukonde alisema amefurahia kusajiliwa na kuwa miongoni mwa kikosi cha Yanga na atahakikisha anaisaidi timu hiyo kufikia malengo yao ikiwamo Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa.

"Nimefurahi sana kuwa miongoni mwa wachezaji wa Yanga, nimekuja kufanya kazi nitashirikana vizuri na wachezaji wenzangu kufikia malengo yanayotarajiwa na sasa tunahitaji kupambana na kushinda Kombe la Kagame," alisema Ukonde.

Chanzo: ippmedia.com