Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii Namungo bab’kubwa

Namungo Group Data Hii Namungo bab’kubwa

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thobias SebastianMore by this Author HAIJAWAHI kutokea! Namungo imeandika rekodi ambayo haijawahi kuandikwa kwa timu za Tanzania kwenye michuano ya kimataifa kwa kushiriki kwa mara ya kwanza na moja kwa moja kwenda makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Namungo ikishiriki kwa mara ya kwanza Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu na wanafikia malengo yao ya kufuzu hatua ya makundi.

Wamefuzu katika hatua hiyo baada ya kuwaondoa CD de Agosto ya Angola kwa jumla ya mabao 7-5, katika michezo yake miwili ambayo yote walicheza katika Uwanja wa Azam Complex, ule wa kwanza ilishinda mabao 6-2 kisha waliporudiana katikati ya wiki ilipoteza 3-1.

Wauaji wa Kusini hao, wameangukia kwenye Kundi D ikiwa na timu za Raja Casablanca ya Morocco, Pyramids ya Misri na Nkana FC ya Zambia na wataanza kazi ikiwa ugenini kuvaana na Raja katika mchezo utakaopigwa Machi 10.

Safari ya Namungo kwenye michuano hiyo ilianza kwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) na kupoteza mbele ya Simba kwa mabao 2-0 na kiupata tiketi kwa vile Simba ilibeba pia ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kuanza kazi dhidi yav Wasudani Kusini na Sudan na kote ikapeta.

Ndipo wakakutana na Primiero de Agosto na kuwang’oa na sasa wapo makundi ikiwa timu ya pili kufika hatua hiyo kutoka Tanzania baada ya Yanga iliyotinga hatua hiyo mwaka 2016 na 2018.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz