Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hesabu za ubingwa kwa Simba, Yanga

49692 UBINGWA+PIC

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

YANGA imebakiza mechi 10, Simba 17 na Azam FC 10 za Ligi Kuu Bara kujua mbivu na mbichi ya nani atachukua ubingwa msimu huu ambao una mzunguko wa mechi 38 kwa uwepo wa timu 20.

Yanga inayoongoza ligi kwa pointi 67 imepoteza pointi 13 zilizotokana na kufungwa na Stand United, Simba na Lipuli, sare zao wakitoka na Ndanda FC, Coastal Union, Simba na Singida United, katika mechi 28 walizocheza wameshinda 21.

Simba ndio inayoongoza kwa viporo wakiwa na mechi 17 mkononi ambazo zitaamua kutetea ubingwa ama kuuachia kwa Yanga au Azam FC, Wanamsimbazi hao wamedondosha pointi sita baada ya kufungwa na Mbao, sare zao zilikuwa dhidi ya Yanga, Lipuli na Ndanda pia wameshinda 17 kati ya 21 walizocheza na wana pointi 54. Kwa upande wa Azam FC wao wamepoteza pointi 17 sawa na mechi 17 walizobakiza Simba kutetea ubingwa, walifungwa tatu, sare nane, hata hivyo walishinda 17 kwa mechi 28 walizocheza na wanamiliki pointi 59.

Ukichana na vita ya ubingwa, kazi nzito ipo kwenye timu zinazopigania kubaki kwenye ligi hiyo, African Lyon imebakiza mechi saba, imecheza mechi 31 yenye pointi 22, Biashara wamecheza michezo 29, wamebakiza tisa wanamiliki pointi 30.

Kwa upande wa Singida United, imecheza mechi 30, imebakiza tisa na ina pointi 33, huku Ruvu Shooting imebakiza mechi saba imecheza 31 inamiliki pointi 35.

KAULI ZA WADAU

Kocha wa Ruvu Shooting ambayo ipo nafasi ya 17, Abdulmutik Haji alijihakikishia timu hiyo kubaki ligi kwa madai mechi nyingi wanazocheza wao ndio watakuwa wenyeji. “Tukishinda mechi moja tutapanda mpaka nafasi ya saba kwani, tutakuwa na pointi 38,” alisema.

Aliyekuwa Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ alisema kwa msimamo wa ligi ulivyo hesabu makini ndizo zitakazoamua nani bingwa ama kushuka daraja.

“Ni sawa Yanga wamepoteza pointi 13 swali ni je watashinda mechi zao zote, hapo ndipo mtihani uliopo, pia Azam huwezi kuweka nje ya ubingwa inaweza ikashinda mechi zote na hao wakapoteza,” alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz