Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hayawi hayawi yamekuwa! Banda afunga pingu za maisha

9572 Pic+banda TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

BEKI wa zamani wa Simba, Abdi Banda leo Jumatano asubuhi amefunga ndoa na mchumba wake Zabibu Kiba, ndo iliyofungishwa na kaka yeka Zabibu, Alli Kiba.

Ndoa hiyo imefungwa asubuhi ya saa 12 katika msikiti wa Ahmad Al Maseeid uliopo Tabata Sanene jijini Dar es Salaam na jioni ya leo Jumatano itafuta sherehe upande wa mwanamke itakayofanyika ukumbi wa Lamada, Ilala Boma.

Banda ambaye kwasasa anacheza soka la kulipwa katika timu ya Baroka FC ya Afrika Kusini atafanya sherehe kubwa upande wao itakayofanyika Jumamosi ya wiki hii kwenye ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort, jijini Tanga ambako ndiyo nyumbani kwa akina Banda.

Mjomba wa Banda, Abdul Bosnia alisema kila kitu kuelekea sherehe hiyo kinakwenda vizuri.

"Tunamshukuru Mungu kijana wetu amefanikisha jambo hili kubwa na zito, ni jambo la kheri na la kumpendeza Mungu, tunawoambea maisha mazuri na yenye furaha katika ndoa yao.

"Ndoa imefungwa lakini shughuli yetu itakuwa Tanga, hivyo tukimaliza upande wa mwanamke ambao sisi ni waalikwa tutakwenda Tanga kwa ajili ya kuhitimisha, kila kitu kinakwenda vizuri," alisema Bosnia.

Chanzo: mwananchi.co.tz