Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatma ya Grealish kujulikana baada ya Euro 2020

Jack Grealish

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Mabingwa wa England Manchester City bado haijafanya mazungumzo na klabu ya Aston Villa juu ya kutaka kumsajili kiungo wa timu hiyo Jack Grealish, isipokuwa wanaripotiwa kuwa wamepeleka ofa ya kumsajili.

Jana Ijumaa ripoti kutoka nchini England ziliripoti kuwa Manchester City wapo tayari kutoa dau la pauni million 100 kama ada ya uhamisho ya mchezaji huyo ambayo ni zaidi ya billion 321 kwa pesa za kitanzania, lakini bado hakuna mazungumzo yaliyofanyika kati ya vilabu hivyo viwili.

Grealish mwenye umri wa miaka 25, alijiunga na Aston Villa akiwa na umri wa miaka 6 na bado anamkataba wa miaka minne na Villa. Klabu hiyo haipo tayari kumuuza mchezaji huyo, huku kukiwa na taarifa kuwa wanataka kuuboresha mkataba wake wa sasa katika harakati za kuhakikisha anabaki klabu hapo.

Inaaminika kwa sasa Manchester City watasubiri mpaka michuano ya Euro 2020 imalizike ndipo wataanza tena harakati za kumuwania kwa sabaabu mchezaji huyo ni sehemu ya michuano hiyo akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya England.

Chanzo: eatv.tv