Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatima ya Ajibu Simba Jumatatu

99235 Ajib+pic Hatima ya Ajibu Simba Jumatatu

Sat, 30 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MBIVU na mbichi kuhusiana na kiungo wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, Ibrahim Ajib, itajulikana keshokutwa, imeelezwa.

Ajibu aliondolewa katika kambi ya vinara hao wa Ligi Kuu Bara baada ya kuchelewa kufika kwenye mazoezi yaliyoanza Jumatano.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, alisema baada ya mchezaji huyo kuchelewa, aliondolewa kwenye kikosi kutokana na kosa la uchelewaji.

"Ajibu si sehemu ya kikosi chetu kwa sababu alichelewa kufika katika siku ya kwanza ya mazoezi Jumatano, atarejea Jumatatu kama mambo yatakwenda vizuri," alisema kocha huyo.

Aliongeza kuwa kikosi chake kinaendelea vema na mazoezi na amekuwa na programu za aina tatu tofauti, lakini amefurahi kufahamu tarehe rasmi ya kurejea kwa ligi hiyo.

Aliwataja wachezaji watatu ambao bado hawajaripoti ni Francis Kahata, Clatous Chama na Sharaf Shiboub, ambaye kwao Sudan bado wako kwenye 'lockdown' kubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live