Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatima nyota wageni yanukia

6407 Dk Mwakyembe Hatima nyota wageni yanukia

Tue, 23 Jun 2020 Chanzo: Hatima nyota wageni yanukia

SERIKALI imesema itatoa mwongozo kuhusu wachezaji wa kigeni watakaoruhusiwa kusajiliwa na timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara hivi karibuni, imeelezwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema ni lazima uandaliwe utaratibu wa kuruhusu wachezaji hao wa kigeni ambao unalenga zaidi kukuza vipaji vya nyota wazawa.

Mwakyembe alisema serikali haitakubali kuona wachezaji wasiokuwa na viwango wanasajiliwa na klabu za hapa nchini kwa sababu uamuzi huo unawanyima nafasi wachezaji Watanzania ambao wanaibukia.

"Ukiruhusu kila mchezaji aje, hatutakuza vipaji vya vijana wetu wanaochipukia kila mwaka, tutatoa uamuzi hivi karibuni, sisi ndio tunaotoa vibali, lazima tuwe na vigezo, sio tukubali tu, tutajadiliana ili kufikia uamuzi utakaokuwa na faida kwetu," alisema Mwakyembe.

Waziri huyo pia amezishauri Simba na Yanga kufanya tathmini mpya ili kupata thamani halisi za klabu hizo kongwe hapa nchini.

Alisema haamini kama Simba ina thamani ya Sh. bilioni 20, na kuelekeza klabu hizo kutumia kampuni za kimataifa ili kutekeleza mchakato huo huku zikiendelea na taratibu za kubadili mfumo wa uendeshwaji.

Chanzo: Hatima nyota wageni yanukia