Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hata Mtibwa Sugar yaweza kupindua matokeo

32892 Pic+mtibwa Tanzania Web Photo

Sat, 22 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Dakika 90 za mchezo wa marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya KCCA ya Uganda kwenye Uwanja wa Azam Complex zinatosha kuifanya Mtibwa iitikise Afrika leo.

Pamoja na kufungwa mabao 3-0 ugenini wiki iliyopita, Mtibwa inaweza kuwatupa nje KCCA kwa kupata ushindi wa idadi kubwa ya mabao au hata ule wa mikwaju ya penati lakini hilo litategemeana na jinsi wawakilishi hao wa Tanzania watachanga karata zao kwenye mechi hiyo.

Hesabu na mbinu sahihi zikichagizwa na nidhamu ya mchezo sambamba na umakini na utulivu wa hali ya juu vinaweza kuifanya Mtibwa Sugar ipindue matokeo na hata kuitoa KCCA ingawa wengi wanaonekana kutowapa nafasi ya kufanya hivyo.

Kocha wa Mtibwa Sugar, Zubeir Katwila alisema wamejipanga kuhakikisha wanapindua matokeo ya mechi ya kwanza ili kupata matokeo ya kusonga mbele.

Katwila alisema wamepoteza mechi ya kwanza kwa makosa ya kawaida ambayo haswa waliyafanya kipindi cha pili na hayo ndio yalitugharimu.

Alisema kwa siku tatu hadi nne wameyafanyia kazi yote hayo ili kuingia kivingine katika mechi ya kesho na kupindua matokeo.

“Haitakuwa kazi rahisi kwetu kupindua matokeo ila wachezaji wangu nimewambia na kuwaelekeza wanatakiwa kupambana dakika zote 90 ili kulifanikisha hilo,” alisema. Mtibwa katika mechi ya kwanza dhidi ya KCCA walipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 na ili wasonge mbele katika hatua inayofata wanatakiwa kushinda mabao 4-0 katika mechi ya kesho uwanja wa Azam Complex.

Muhimu kwa Mtibwa Sugar

Jambo muhimu ambalo Mtibwa wanapaswa kulifanya kwa dakika zote za mchezo leo, ni kuhakikisha wachezaji wake wanakuwa na nidhamu nzuri ya kujilinda na kushambulia ili kutowapa mwanya wapinzani wao kuwamaliza.

Moja ya makosa makubwa ambayo Mtibwa wanapaswa kuyaepuka leo ni wachezaji wake kukosa nidhamu ya kujilinda pindi wanaposhambuliwa jambo ambalo ndilo lilichangia wapoteze mchezo wa kwanza ugenini.

Wachezaji wa Mtibwa mara kwa mara huwa hawafiki na wanawakaba kwa macho ilhali wenzao wa KCCA jambo ambalo liliwafanya wapinzani wao kuwa na uhuru mkubwa kila walipofanya shambulizi langoni na wawakilishi hao wa Tanzania na kufanikiwa kufunga mabao matatu. Kingine ambacho Mtibwa wanapaswa wakifanye leo ni kuhakikisha nyota wake wa safu ya ushambuliaji wanakuwa na umakini wa kutumia kila nafasi wanayoipata ndani ya eneo la hatari la KCCA kupiga mashuti kwa akili na kufunga mabao.

Ni jambo linalopaswa kufanywa mapema kuanzia dakika za mwanzoni ili kuwachanganya wapinzani wao vinginevyo wanaweza kujiweka kwenye wakati mgumu.

Haitokuwa jambo la kushangaza kwa Mtibwa Sugar kuwatoa KCCA kwani kuna kundi kubwa la timu ambazo zimewahi kupindua matokeo na kufuzu hatua inayofuata licha ya kuchapwa idadi kubwa ya mabao kwenye mechi ya kwanza.

Mwaka 1979, Simba ilichapwa nyumbani Tanzania kwa mabao 4-0 na Mufulila kwenye hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini kwenye mchezo wa marudiano huko Zambia ilishinda kwa mabao 5-0.



Chanzo: mwananchi.co.tz