Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hat-trick yampeleka Nchimbi Stars

78457 Pic+nchimbi

Fri, 4 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

BAADA ya kuifunga Yanga mabao matatu 'hat-trick' mshambuliaji wa Polisi Tanzania, Ditram Nchimbi ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' kinachotarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda.

Nchimbi ambaye hii ni mara yake ya kwanza kuitwa Stars ameungana na nyota wengine 28 waliotajwa jana Alhamis na kaimu kocha mkuu wa Stars, Etienne Ndayiragije kujiandaa na mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 14 mwaka huu mjini Kigali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kupitia Ofisa Habari wao, Cliford Ndimbo imesema kikosi hicho kinatarajia kuingia kambini hivi karibuni kujiandaa na mchezo huo ambao upo kwenye kalenda ya FIFA.

Imeelezwa kwamba mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Rwanda kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano wa CHAN dhidi ya Sudan unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 18 mwaka huu.

Nchimbi amepata nafasi hiyo baada ya kuonyesha kiwango kizuri na kufunga mabao matatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu huku akiingia kwenye historia ya kuwa mshambuliaji wa kwanza kufunga hat-trick ambapo timu yake ilitoka sare ya bao 3-3

Nyota wengine walioitwa kwenye kikosi hicho ni Juma Kaseja, Metacha Mnata, Said Kipao, Salum Kimenya, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Mohamed HJussein, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Bakari Nando, Himid Mao, Jonas Mkude, Kelvin John

Farid Mussa, Adi Yusuph, Idd Suleiman, Mudathir Yahya, Salum Abubakari, Frank Domayo, Mzamiru Yassin, Shaban Idd, Ayub Lyanga, Abdul Aziz Makame, Andrew Suimchimba, Miraji Athuman, Feisal Salum, Mbwana Samatta na Saimon Msuva.

Chanzo: mwananchi.co.tz