Kwa muda mrefu kulikuwa na tetesi kuwa staa wa Tottenham Hotspurs Harry Kane ni shabiki wa Arsenal toka enzi zake za utoto, ikiwa ni siku moja imepita toka Harry Kane aingie kwenye rekodi ya kuifungia Tottenham Hotspuras magoli 100.
Kane akiwa na umri wa miaka 8 aliachwa katika timu ya watoto ya Arsenal kabla ya baadae kipaji chake kuonekana kikubwa, taarifa ikufikie staa huyo mwenye umri wa miaka 24 sasa anaingia katika rekodi ya kuwa mchezaji wa pili Ligi Kuu England katika kipindi cha miaka 100 kufunga magoli 100 kwa haraka baada ya Alan Shearer.
Goli la penati la Harry Kane alilolifunga dhidi ya Liverpool katika mchezo wa jana linakuwa ni goli lake la 100 EPL kufunga na ameingia katika rekodi ya kuwa mchezaji wa 27 wa Spurs kufunga magoli 100 katika EPL.
VIDEO: John Bocco na Mzamiru Yassin walivyoifungia Simba leo vs Ruvu Shooting