Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harry Kane kusepa Tottenham Hotspurs

HARRY KANE 1 Harry Kane kusepa Tottenham Hotspurs

Tue, 18 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Nahodha na mshambuliaji tegemeo wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane ameibuka upya kujadili hatma yake klabu hapo kwa kukiri wazi kuwa ndoto yake kwa sasa ni kutaka kushinda mataji makubwa baada ya kusubiri kwa muda mrefu na Spurs kushindwa kufanya hivyo.

Submitted by George David on Jumanne , 18th Mei , 2021 Nahodha na mshambuliaji wa Spurs, Harry Kane akiwa anapiga penalti kufunga bao dhidi ya Everton msimu huu.

Kane ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo wakati alipokuwa anafanya mahojiano na kituo cha Sky Sports nchini England. Kane amesema;

“Nataka kuanza kushinda mataji makubwa na klabu. Hatufanyi hivyo kwasasa. Ni chungu tamu, lakini ndivyo ilivyo. Najivunia kuwahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kwani umekuwa msimu mzuri uwanjani”.

“Nikiangalia mwisho wa maisha yangu ya soka, hivi ndiyo vitu ambavyo nitakuwa najivunia zaidi, lakini lengo kwasasa kama mchezaji ni kushinda mataji”.

Hii ni mara ya pili Kane kuzungumzia ndoto yake ya kutaka kushinda mataji jambo linaloonekana limeshindikana ndani ya klabu yake hivyo na kudhihirisha kuwa anataka kutoka klabuni hapo na kujiunga na klabu ambayo inaweza kumsaidia kutimiza ndoto yake hiyo.

Tayari vilabu vya jiji la Manchester, Manchester City, Manchester United na matajiri wa jiji la London, klabu ya Chelsea wanahusishwa kiukaribu kuwania saini ya mkali huyo wa kufumania nyavu EPL.

Tokea kuanza kwa msimu huu, tayari Kane amefunga mabao 22 na kufungana na Mohamed Salah wa Liverpool wawili hao wakiwa vinara wa upachikaji mabao mpaka sasa wakiwania kiatu cha dhahabu kwenye ligi hiyo pendwa Duniani.

Kane mwenye umri wa miaka 27, amecheza michezo 47 kwenye michuano yote msimu huu akiwa na klabu yake ya Spurs, na amefanikiwa kufunga mabao 32 na kutengenza 16 huku akiwa ameshacheza michezo 334, mabao 220 na assisti 46 tokea atue Spurs miaka 6 iliyopita.

Kane anakadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 120 za Uingereza ambaoz ni sawa na zaidi ya Bilioni 330 za Kitanzania kama ada ya uhamisho kwa timu itakayohitaji saini ya kiboko huyo wa kuweka mpira kimiani.  

Chanzo: eatv.tv