Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harry Kane ashika nafasi ya pili ya wachezaji waliofikisha magoli 100 kwenye ligi kuu Uingereza

2644 4222853 TZW

Tue, 6 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Harry Kane atimiza idadi ya magoli 100 katika Ligi Kuu  ya uingereza baada ya kuweza kushinda penati ya pili katika mechi ya  Tottenham dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili jana.



Mshambuliaji huyo wa Uingereza amekuwa mchezaji wa pili  kufikia hatua kubwa zaidi akiwa nyuma ya Alan Shearer,baada ya kusawazisha goli dakika za mwisho huko Anfield na kufanya watoke sare ya 2-2 na Liverpool.



Kane, alipatwa na ujasiri wa kugonga nyuma ya wavu baada ya kukosa penati ya kwanza ambayo ingeweza kuwafanya Spurs kupata uongozi wa 2-1.

Mbali na hayo Kane alisema kwamba alikuwa  tamaa ya kufunga mara baada tu ya kipa  wa Liverpool Loris Karius kuokoa penati na pale ambapo  Mohamed Salah alipofunga goli lake la pili katika mchezo huo na kuwafanya Liverpool kuwa mbele katika  dakika ya 91.



Kane, ambaye alifunga bao lake la 22 la msimu huu na pia la 100 katika  mechi 141 alizocheza kwenye Ligi kuu ya Uingereza , aliiambia  Sky Sports Main kuwa  “Nilikuwa nikiomba.

“Hutarajii hasa wakati wa  dakika za mwishoni  lakini nina shukuru sana baada ya kupata nafasi ya pili na nina furahi sana kufikisha idadi ya  magoli 100 katika Ligi Kuu na nina furaha sana ya kuwa miongoni mwa wachezaji kufikisha magoli  100.”



Kampuni ya Nike wamemtengenezea kiatu  cha kipekee kiitwacho Nike Hypervenom 3 HK ambacho atakivaa  Kane katika mechi yake ijayo. Viatu 100 ndiyo idadi ya viatu hivyo vilivyo tegenezwa na vina  rangi nyeupe na rangi ya bluu na  zitapatikana madukani hapo  baadaye.



 



Kane amekuwa  mchezaji wa 26 kufikisha idadi ya magoli  100 katika Ligi Kuu ya Uingereza akiwa mbele ya Sergio Aguero katika orodha ya hiyo.

Alan Shearer

Alan Shearer ambaye ndiye anayeongoza orodha hiyo alifunga goli lake la 100 ndani ya mechi 124 tu.  ndani ya mechi 160 na Ian Wright ndani ya mechi 173.

Thierry Henry

Ian Wright

Na Raheem Rajuu
Chanzo: bongo5.com