Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hapa Yanga na Azam, kule Simba na Mtibwa hapatoshi Chamanzi

63255 Pic+vijana

Tue, 18 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mashindano ya Vijana chini ya miaka 20, yamefikia katika hatua ya nusu fainali kwa kuzikutanisha timu za Yanga dhidi ya Azam, Simba na Mtibwa Sugar.

Katika nusu fainali ya kwanza utachezwa mchezo wa Yanga dhidi ya Azam huku wa pili ukiwa Mtibwa Sugar na Simba.

Mchezo wa Yanga na Azam utapigwa Saa kumi jioni (10:00) huku Mtibwa na Simba wakicheza Saa 1:00 usiku michezo yote inapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Akizungumzaia mechi yake Kocha Nico Kiondo wa Simba, alisema anatambua ugumu wa mchezo wao dhidi ya Mtibwa, lakini hawatokubali kupoteza.

"Timu haina mchezaji yeyote majeruhi kwahiyo tunaenda kupambana kusaka ushindi na kusonga mbele katika mashindano haya," alisema Kiondo.

Aliongeza wamekuwa na wakati mgumu mara kwa mara pindi wanapokutana na Simba katika mashindano ya vijana.

Pia Soma

Naye kocha wa Mtibwa Sugar, Vicent Barnabas alisema hawajali matokeo ya zamani waliyokuwa wakiyapata dhidi ya Simba.

"Tunataka ushindi na sio kitu kingine lakini sionkwa kufata historia, hizo tushasahau na sasa tunaangalia namna ambavyo tunaweza kupata ushindi kwani ndio matarajio yetu," alisema.

Katika michezo ya mwishoYanga alimfunga 1-0 Ruvu Shooting, Simba 1-1 kagera Sugar, Azam 2-1 prison.

Chanzo: mwananchi.co.tz