Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hao Yanga, KMC mzuka umepanda kinoma kucheza kimataifa

61404 Pic+yanga

Thu, 6 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Muda mfupi baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuzitaja Yanga na Azam kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao, wadau wa michezo wametoa maoni tofauti.

Yanga inatarajiwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na KMC itacheza Kombe la Shirikisho.

Timu hizo zimebebwa na rekodi ya Simba msimu uliopita ambapo ilifika hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo kuipa fursa Tanzania kuongeza timu nyingine mbili katika michuano ya kimataifa msimu ujao.

Wakati Yanga itaungana na Simba, kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, KMC itashiriki Kombe la Shirikisho sawa na Azam.

Yanga

Akizungumza jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omari Kaya alisema kupewa nafasi ya kushiriki michuano hiyo ni fursa kwa klabu hiyo, hivyo wataitumia kikamilifu. “Tumesikia taarifa ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini tunasubiri ya maandishi. Lakini hilo ni jambo jema kwa Klabu ya Yanga,” alisema Kaya.

Pia Soma

KMC

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta alisema hawatakuwa wanyonge kwenye mashindano ya kimataifa na ameishukuru Simba kuwabeba.

“Ndoto nyingine ya KMC imetimia, awali tulikuwa na ndoto ya kupanda kucheza Ligi Kuu na kufanya vizuri, imewezekana na sasa tunakwenda hatua nyingine ya kushindana kimataifa, hatuwezi kuwa wanyonge,” alisema Sitta.

Alisema wataimarisha kikosi chao kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa kwa kuwa inakutanisha wachezaji wenye viwango bora.

“Japo hatuna matarajio makubwa, lakini hatuwezi kuondoshwa katika hatua za awali au kuishia kufungwa mabao matano na kuendelea, tutaimarisha kikosi chetu kwa kuongeza wachezaji ambao wana uwezo wa kupambana kimataifa,” alisema Sitta.

Wadau walonga

Mchambuzi Ally Mayay alisema ni vyema timu zote zilizopata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao 2019/2020 kuanza mapema kujenga timu imara.

“Maandalizi yanatakiwa kuanza sasa sio kusubiri baada ya kutolewa kwa ratiba, wanatakiwa kusajili kutokana na uhitaji wa vikosi vyao, itapendeza kuona ushindani wa timu za Tanzania ukiendelea kuwa mkubwa katika mashindano hayo kama walivyofanya Simba msimu uliopiota,” alisema Mayay.

Kocha Kenny Mwaisabula, alisema wenye uzoefu na mashindano hayo wanatakiwa kujiongeza kwa kuboresha vikosi vyao ili kufika mbali zaidi tofauti na msimu uliopita.

Kanali mstaafu Idd Kipingu, alisema kuingiza timu nne kwenye mashindano ya kimataifa msimu ujao ni baraka kwa taifa, klabu na wachezaji wenye kutambua umuhimu na faida ya mashindano hayo.

“Nasikitika kuona hatuna mipango ya kuzalisha wachezaji wengi wa kizawa, endapo ingekuwepo basi kusingekuwa na hajaya kufauta wachezaji nje ya nchi, Simba, Yanga na Azam wanaweza kutumia fedha zao vipi kuhusu KMC na wengineo.

“Siku hizi mpira hauchezwi kabisa mashuleni ambako ni chimbuko la mpira wetu kidogo mitaani umekuwa ukichezwa. Nachoweza kushauri   wachezaji wetu ni kuonyesha vipaji vyao kwa sababu huko ndipo wanapoweza kutokea kwa wepesi,” alisema Kipingu.Kauli ya TFF

Mapema jana TFF ilisema CAF imeongeza timu za Tanzania baada ya kuingia katika orodha ya timu 12 bora kwenye viwango vya shirikisho hilo.

Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu zilizofanyiwa marekebisho na Kamati ya Utendaji baada ya kupatikana nafasi nne, Tanzania itawakilishwa na Simba, Yanga, Azam na KMC.

“Kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu zilizofanyiwa marekebisho na Kamati ya Utendaji baada ya kupatikana  nafasi nne timu za Tanzania zitakazowakilisha kwenye mashindano hayo ni Simba, Yanga, Azam na KMC Kombe la Shirikisho (CAF CC).”

Chanzo: mwananchi.co.tz