Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamilton kuvunja ukimya Ijumaa hii

Lewis Hamilton 1024x683 Lewis Hamilton

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Bingwa mara 7 wa Dunia wa Formula One Lewis Hamilton ataongea kwa mara ya kwanza Mubashara kwenye televisheni ijumaa hii tangu alipoukosa ubingwa wa msimu uliopita mbele ya Max Max Verstappen mwezi Novembe mwaka 2021.

Hamilton na timu nzima ya Mercedes Benz wakiongozwa na bosi wa timu hiyo Toto Wolff wataongea siku ya Ijumaa Februari 18 watakapokuwa wakitambulisha gari zao mpya watakazozitumia msimu huu wa 2022, lakini pia wataelezea baadhi ya vitu vya kiufundi walivyovibadilisha kutoka msimu uliopita kueleka msimu huu.

Shahuku ya watu wengi keelekea siku ya ijumaa ni kutaka kujua msimamo wa Hamilton juu ya kile ambacho kilitokea kwenye mbio za  mwisho za msimu uliopita za Abu Dhabi ambazo zilimfanya akaukosa ubingwa wa msimu uliopita na ilikuwa ikiripotiwa kuwa baada ya kuukosa ubingwa alipanga kustaafu  kukimbiza magari ya Lang langa.

Taarifa za dereva huyo wa Mercedes raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 37 kustaafu zilivuma zaidi baada ya mbio za Abu Dhabi kumalizika kwa utata mkubwa baada ya dereva wa Red Bull Max Versappen kumpita Hamiliton kwenye eneo ambalo kikanuni haikutakiwa kuwa hivyo na kumfanya Max kuibuka bingwa kitendo ambacho kilimchukiza sana Lewis.

Sasa ni rasmi Hamilton ataliwinda taji la 8 la Formula One ili kuweka rekodi yakuwa dereva aliyeshinda ubingwa wa michuano hii mara nyingi zaidi, kwa sasa analingana na Michael Schumacher wote wakiwa wameshinda mara 7. Na msimu huu wa 2022 wa Formula One utaanza Machi 20 na utamalizika Novemba 20, 2022.

Chanzo: eatv.tv