Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamilton amekanusha taarifa za kustaafu

Lewis Lewis Hamilton, atauwania ubingwa wa 8 wa Formula One msimu huu 2022

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Lewis Hamiliton amethibitisha kuendelea kukimbiza magari kwenye Lang langa msimu huu wa 2022 amesema kuwa hakuwahi kusema kuwa anastaafu. Dereva huyo wa Mercedes amesema haya wakati wa uzinduzi wa magari maya watakayo yatumia msimu huu.

Hamilton ameongea na vyombo habari kwa mara ya kwanza leo tangu alipoukosa ubingwa wa Formula One msimu uliopita mbele ya Max Verstappen wa Red Bull, kwenye mzinguko wa mwisho kwenye mbio za Abu Dhabi mwezi Novemba mwaka jana.

"Sijawahi kusema nitaacha. Ninapenda kufanya ninachofanya, ni fursa kwangu. Unajisikia kama familia hakuna hisia kama hii. Ulikuwa wakati mgumu kwangu, nilihitaji kupumzika kidogo, nikizingatia zaidi wakati huu, na familia yangu na kuwa na wakati mzuri." Amesema Hamilton 

Hamilton anathibitisha kuwa hakutaka kustaafu ikiwa ni siku moja tu imepita tanga uongozi wa Formula One ulipotangaza kumuondoa Michael Masi kama Mkurugenzi wa kuongoza magari ya Langa langa (Race Director).

Ili ripotiwa kuwa endapo kama Masi raia wa Australia mwenye umri wa miaka 44 angeendelea kuongoza mbio hizo basi Hamiliton angestaafu. Michael Masi alishambuliwa na timu ya Mercedes kuwa aliwanyima haki kwenye mbio za mwisho msimu uliopita za Abu Dhabi kwa kumruhusu Max Verstappen kumpita Lewis eneo ambalo haukipaswa kuwa hivyo kikanuni. Baada ya tukio hilo Mercedes walionekana kushinikisha aondolewe kwenye nafasi hiyo.

Baada ya Masi kuondolewa kama muongoza magari kwenye Langa langa (Race Director) nafasi yake imechukuliwa na watu wawili ambao watasaidiana Niels Wittich na Eduardo Freitas.

Msimu huu timu ya Mercedes Benz inaongozwa na timu ya Madereva Lewis Hamilton na George Russell. Na Hamilton mwenye miaka 37 atakuwa akiuwinda ubingwa wa 8 wa Formula One.

Chanzo: eatv.tv