Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Manara kubaki CCM baada ya Man United kushinda

4558 165ec686 Df57 4e53 B5f8 95ff9a300db3 TZW

Mon, 12 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2 – 1 dhidi ya Liverpool mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliyopigwa katika dimba la Old Trafford.



Kufuatia ushindi huo unamfanya afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara kusalia katika chama chake cha Mapinduzi (CCM) hii ni kutokana na ahadi yake aliyo itoa katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuwa endapo timu yake hiyo pendwa ya United ingefungwa na Liverpool basi angekihama chama hicho na kujiunga na  chama cha Hashim Rungwe cha Chauma.

Ikitokea Liverpool kuifunga Manchester nahama CCM najiunga na chama cha Hashim Rungwe ..hawatufungi hata kwa bahati mbaya.

Liverpool ikiifunga Manchester nahama CCM – Haji Manara



Katika mchezo huo mshambuliaji wa Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza, Marcus Rashford amefanikiwa kuisaidia United kuchomoza na ushindi baada ya kufunga mabao mawili huku Eric Bailly akijifunga na kuifanya mechi hiyo kumalizika kwa matokeo hayo ya mabao 2 – 1.

Kwa matokeo hayo sasa Manchester United inaendelea kusalia katika nafasi ya pili kwakuwa na jumla ya pointi 65 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Manchester City wenye alama 78.

Chanzo: bongo5.com