Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Manara amfungukia Niyonzima

Fri, 9 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ya klabu ya Simba, Haji Manara ameelezea hali ya majeruhi inayomkabili kiungo wa kimataifa wa Rwanda na timu hiyo, Haruna Niyonzima.



Manara amesema kuwa Niyonzima anatarajiwa kupelekwa nchini India kwaajili ya matibabu ya majeraha yake yanayo mkabili.

“Haruna anatarajiwa kuelekea India ndani ya sikumbili hizi kwaajili ya matibabu, atakuwa na operesheni ndogo kwenye mfupa wa paji la mguu,”amesema Manara.

Manara ameongeza “Atakaa huko kwa muda wa siku mbili, tatu na atatumia muda wa wiki tatu hadi anarejea uwanjani.”

“Majeraha yake yameanza muda mrefu hata kabla ya kujiunga na Simba lakini kama mchezaji wetu tunahakikisha tunampeleka India na anatarajiwa kurejea mwezi Machi akiwa fiti na tayari kwaajili ya kuitumikia klabu yake.”

Chanzo: bongo5.com