Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Manara amewasikia wanaoibeza Simba kutoka sare ya 2-2 vs Mwadui FC

3422 Sequence 01.Still051 TZW

Mon, 26 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Baada ya wekundu wa msimbazi Simba kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu jana dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga na kutoka sare ya kufungama magoli 2-2 maneno yamekuwa mengi na watu wameanza kukosoa kuwa Simba imepunguza kasi ya Ubingwa.

Kupitia ukurasa wake wa instagrama afisa habari wa Simba Haji Manara ameamua kuandika ujumbe wa wazi kwa wanaoibeza Simba kwa matokeo hayo na kusihi wana Simba kuwa watulivu kuwa hakuna timu ambayo haiwezi kupata sare duniani.

“Salaam zangu za Ijumaa  baada ya matokeo ya jana mengi yamesemwa moja wapo eti tushayumba,,hayo ni maneno yanayotoka kwa watu walewale ambao wanaamini zama ni hizi hizi na Mungu ni wao peke yao…..wapuuzeni”

“Mwadui imezifunga Singida United na kabla yetu sisi waliwafunga Mtibwa 3-1 kule Shinyanga..wametoka sare na Yanga na Azam tena wakiwa kwao Dar..hizo ndio big five kwenye ligi kwa sasa,,sisi kutoka nao sare kwao why iwe nongwa tena ugenini?”

“Simba haitatoka mstarini na washabiki wetu tulieni na wajibu wenu ni kuiombea timu na kuisuport…msicheze ngoma ya wachimvi……. Lakini pia kwa mashabiki wetu muelewe timu yetu bado inaongoza ligi na hatujafungwa bado…haitatokea duniani timu isitoke hata droo.hata tukimsajili Ronaldo na Messi”

“Msisahau Mwadui hawa hawa walisababisha Mkwasa atake kupigwa na washabiki wa Yanga baada ya kutoka nao sare hapa jijini Niwajuze pia hali ya Boko inaendelea vema kwa sasa na jopo la madaktari linahangaika nae ili aweze kucheza tena haraka iwezekanavyo Ijumaa Kareem

Chanzo: millardayo.com