Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Manara ametangaza kikosi chake bora VPL round ya kwanza

2364 7uc3Ow7.png

Thu, 1 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Ligi Kuu Tanzania bara round ya kwanza msimu wa 2017/2018 imemalizika kwa wekundu wa Msimbazi kukaa kileleni wakiwa na jumla ya point 35 wakifuatiwa na Azam FC wenye point 30, leo January 31 ukiwa mzunguuko wa kwanza umemalizika.



Afisa habari wa Simba Haji Manara ametaja kikosi chake bora katika Ligi Kuu Tanzania bara, kwa wachezaji waliofanya vizuri katika mzunguuko wa kwanza, kikosi hiki kinahusisha jumla ya wachezaji 11 kutoka timu mbalimbali za Ligi Kuu.



Kwa mujibu wa Haji Manara kikosi chake bora ndio hiki, golikipa ni Aishi Manula kutoka Simba, beki namba Erasto Nyoni kutoka Simba, namba tatu Shafiq Batambuzi kutoka Singida United, mabeki wa kati ni Asante Kwasi kutoka Simba, Yakub Mohamed kutoka Azam FC.

Winga ya kulia Shiza Kichuya kutoka Simba, winga ya kushoto ni Emmanuel Okwi kutoka Simba, Wakati viungo ni Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Yanga, Said Ndemla kutoka Simba na washambuliaji Obrey Chirwa wa Yanga na John Bocco.

Baada ya hapo Haji Manara akaambatanisha kikosi hicho na maelezo haya “Hiki ni kikosi changu bora kwenye mzunguko wa kwanza wa VPL..nimezingatia mchango wa mchezaji binafsi kwa timu yake,haya ni mawazo yangu huru,wapingaji mje na data”

Manara baada ya Yanga kupata penati “Baadhi ya maamuzi ni kichefuchefu”

Chanzo: millardayo.com