Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

HIVI NDIYO YANGA WALIVYOWEZA KUIBUKA NA USHINDI

Capture 649?fit=572%2C403 HIVI NDIYO YANGA WALIVYOWEZA KUIBUKA NA USHINDI

Thu, 14 Jan 2021 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi, amemkabidhi kombe la ushindi nahodha wa Timu ya Yanga Sc Haruna Niyonzima katika mchezo wa Fainali ya Mapinduzi Cup uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Stadium visiwani Zanzibar ambapo timu ya Yanga Sc ilishinda kwa mikwaju ya Penati 4-3 kufuatia dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa sare ya 0-0

Vile vile Rais wa Zanzibar ametoa medali za Dhahabu pamoja na kuwakabidhi shilingi milion 15 kwa bingwa wa Fainali ya michuano hio ambao ni Yanga Sc huku mshindi wa pili ambao ni Simba Sc mbali na medali, wamezawadiwa fedha taslimu, shilingi milioni 10.

Hiki ni Kikombe cha 2 kwa klabu ya Yanga Sc kushinda ambapo Kombe la Kwanza walishinda mwaka 2007.

Chanzo: zanzibar24.co.tz