Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

HII NDIO SABABU YA KOCHA WA AZAM KUSITISHIWA MKATABA WAKE

Azam+pc HII NDIO SABABU YA KOCHA WA AZAM KUSITISHIWA MKATABA WAKE

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Uongozi wa Klabu ya Azam FC umesema kuwa umefikia makubaliano ya pande mbili na kocha wao Aristica Cioaba, juu ya kusitisha mkataba wake pamoja na Kocha wa viungo, Costel Birsan, wote wakiwa raia wa Romania.

Kwasasa Azam FC imesema timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Bahati Vivier, kutoka Burundi, hadi pale watakapotoa taarifa nyingine.

Pia Azam FC imemshukuru Cioaba na Costel, kwa mchango wao chanya walioutoa kwa kipindi chote walichohudumu ndani ya timu hio na wanapenda kuwatakia kila la kheri popote watakapokwenda.

Cioaba ameingoza Azam FC kwenye mechi 50 za mashindano (Ligi Kuu na Kombe la FA), akishinda mechi 28, sare 11 na kupoteza.

Chanzo: zanzibar24.co.tz