Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gor Mahia nguvu sawa na Rayon

10492 GO.png TanzaniaWeb

Sun, 1 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

TIMU ya Gor Mahia imetoshana nguvu na Rayon Sporst baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.

Gor Mahia walionekana kutawala mchezo vizuri kwani katika kipindi cha kwanza waliweza kuwazidi nguvu Rayon Sports hasa katika eneo la kiungo.

Rayon walionekana kutawala mchezo vizuri na kutengeneza nafasi lakini katika umaliziaji walikuwa wakipata tabu baada ya kukosa mtu sahihi katika safu ya ushambuliaji.

Gor Mahia walianza kupata bao dakika36 kupitia kwa Jacques Tuyisenge aliyeunganisha krosi ya Gukhan Ephrem, huku bao la pili likifungwa dakika 42 na Mieno Humphrey.

Rayon hawakukata tamaa kwani waliendelea kupambana ambapo Dakika 62 walipata bao kwa mkwaju wa penalti.

Rayon baada ya kupata bao walionekana kupata nguvu kwani walikuwa wakiongeza mashambulizi mara kwa mara na Dakika 88 walipata bao la kuchomoa kupitia kwa Patrick Kwizera baada ya kupiga shuti lililotinga moja kwa moja wavuni.

Chanzo: mwananchi.co.tz