Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes hesabu zote kwa Yanga kwanza

Invest Ed Gomes hesabu zote kwa Yanga kwanza

Mon, 3 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Yanga utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Simba juzi usiku ilitinga robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Kagera Sugar, kwa ushindi wa mabao 2-1, shukrani kwa wafungaji, Bernard Morrison na Meddie Kagere.

Akizungumzia na gazeti hili jijini jana, Gomes amewasifu wachezaji wake kutokana na uwezo walioonyesha kwa kutoka nyuma na kusawazisha kabla ya kupata bao la ushindi, lililowaweka katika nafasi nzuri ya kuelekea kutetea ubingwa wao huo.

Alisema walimiliki sehemu kubwa ya mchezo kipindi cha kwanza na kucheza vizuri, lakini hawakuwa na bahati ya kufunga jambo lililomlazimu kufanya mabadiliko ya kiufundi kipindi cha pili ambayo yalizaa matunda.

"Niliamua kubadili mbinu kwa kuwatumia washambuliaji wawili, Meddie Kagere na John Bocco ili kuongeza mashambulizi, upande wa viungo pia nilimuingiza Bernard Morrison, aliweza kutimiza majukumu kwa wakati na kuwafanya Kagera Sugar washindwe kuhimili kasi yetu," alisema Gomes.

Alisema baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali, sasa wanaelekeza nguvu katika mechi ijayo dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, na ni muhimu kushinda kwa kuwa unaamua mustakabali wa ubingwa msimu huu.

“Kuelekea mchezo dhidi ya Yanga sisi morali yetu ipo juu, tumetoka kucheza mechi sita na kushinda zote na mechi hii itaonyesha nani atakuwa bingwa kwa hiyo ni vizuri kushinda mechi hiyo dhidi ya Yanga," alisema Gomes.

Alisema hawezi kuweka wazi mipango yake na kuhusu Morrison ambaye amekuwa mchezaji muhimu kwa kuisaidia timu hiyo kumuanzisha katika mechi ijayo dhidi ya Yanga.

Alisema hana mashaka na uwezo wa Morrison, lakini pia hawezi kuwashutumu washambuliaji wake hasa Kagere kukosa nafasi nyingi, hivyo ana imani atafanikiwa kutumia nafasi na kufunga mabao kwenye mechi zijazo na kuendelea kuwa juu ya kwa ufungaji.

Naye beki wa Simba,Joash Onyango, alisema wanachokifikiria kwa sasa ni mechi yao dhidi ya Yanga na si Kaizer Chiefs ambayo wanacheza nayo kati ya Mei 14-15, mwaka huu.

"Tunashukuru tumeingia robo fainali na sasa hatuwezi kuwazungumzia Kaizer Chiefs wakati tuna mechi nyingine hivi karibuni dhidi ya Yanga, sasa tumemaliza FA tunaenda kujiandaa dhidi ya Yanga," alisema Onyango.

Alisema ana imani itakuwa mechi ya ushindani kwa sababu timu zote zinahitaji matokeo ila kwao watahitaji pointi tatu muhimu kwa ajili ya kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba ambao ni wenyeji wa mchezo huo, ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 61, nne mbele ya Yanga iliyopo mebe kwa michezo miwili.

Chanzo: ippmedia.com