Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes: Tutafanya maajabu

Gomes Pic Data Gomes: Tutafanya maajabu

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KOCHA mkuu wa Simba, Didier Gomes  amesema anatambua ugumu lakini watapindua matokeo katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Kaizer Chiefs  katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba wanahitaji ushindi wa 5-0 ili waweze kutinga hatua ya nusu fainali baada ya mchezo wa kwanza kufungwa 4-0 nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 21 jijini Dar es Salaam, Gomes amesema ana imani kubwa na wachezaji wake kupindua matokeo kutokana morali waliyoionyesha uwanjani.

“Wachezaji wote wanaonyesha uhitaji wa kutaka kucheza mchezo huu, wanajituma uwanjani na lengo ni kuhakikisha tunashinda mchezo huu.”

Gomes amesema mchezo huo ni mgumu na wanatakiwa wapambane kufa na kupona ili kuweza kufuzu katika hatua ya nusu fainai.

“Tumepoteza katika mchezo wa kwanza lakini tunajua tulipoteza kwa staili gani, kwenye mchezo uliopita tulicheza kwa kushambulia na tulimiliki mpira zaidi yao.”

Kocha huyo alisema katika mchezo wa kesho watacheza zaidi ya mchezo wa kwanza na lengo ni kuhakikisha wanapata magoli mengi.

“Tunaenda kucheza kwa kushambulia lakini huku tukijua kwamba nao ni wazuri hivyo tutacheza kwa umakini wa kuzuia pia.”

Aliongeza kwa kusema; ”Tulipoteza kwa mipira ya krosi kweli lakini tumetumia mazoezi yetu kurekebisha makosa katika eneo letu la ulinzi.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz