Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes: Hasira Yanga sasa kwa Kaizer Chiefs

Gomes Ed Gomes: Hasira Yanga sasa kwa Kaizer Chiefs

Mon, 10 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

-Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili, ilikuwa ichezwe saa 11:00 jioni lakini zikiwa zimebaki saa tatu kabla ya mchezo huo kuanza, TFF ilizitaarifu klabu zote mbili kuwa imepokea maagizo kutoka serikalini kupitia wizara husika ya michezo kuwa mechi hiyo isogezwe mbele na kuchezwa saa 1:00 usiku.

Hata hivyo, Yanga iligomea uamuzi huo kuwa ni kinyume cha Kanuni ya 15 (10) ya Ligi Kuu inayohusu taratibu za michezo ambayo inataka mabadiliko yote ya michezo kujulishwa kwa pande zote husika angalau saa 24 kabla ya muda wa awali.

Lakini Gomes akizungumza na gazeti hili jijini jana, alisema walijipanga vizuri kwa ajili ya kuvuna pointi zote tatu ila wameshtushwa na kilichotokea kwa kuwa wote walipokea taarifa muda mmoja, hivyo maandalizi hayo anayageuzia kwa Kaizer Chiefs Jumamosi.

Alisema hawakuwa na namna kwao hasa baada ya kupata taarifa za kusogezwa mbele kwa muda, lakini kikubwa ilikuwa ni jinsi walivyojiandaa.

"Nina imani tulijiandaa vizuri na tulikuja kutafuta pointi tatu, haya mambo mengine ya kubadilisha muda hatuwezi kuona shida kwa sababu hakuna namna, inategemea na jinsi ya timu ilivyojiandaa," alisema Gomes.

Alisema kwa maandalizi waliyoyafanya ana imani mchezo ungekuwa mzuri na mashabiki wao wangepata burudani kutokana na kandanda safi la kuvutia ambalo wangelitandaza.

Aidha, Gomes alisema amesikitikia mashabiki waliojitokeza Uwanja wa Benjamin Mkapa kuangalia mechi hiyo ya watani wa jadi lakini wakashindwa kupata burudani hiyo, wakiondoka nyumbani patupu.

"Unaweza kusema kwamba ni huzuni na masikitiko kuona mashabiki ambao wamejitokeza kutazama burudani, lakini haijawa hivyo. Hamna namna kwetu. Imekuwa ni mshtuko kwa kilichotokea kwa sababu tayari tulikuwa tumejiandaa kwa ajili ya mechi hii," alisema.

Kocha huyo alisema sasa akili na nguvu zao ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Alisema mipango yake ilikuwa mechi dhidi ya Yanga kuwa sehemu yao ya maandalizi ya mchezo wao wa robo fainali ya michuano hiyi mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu.

"Ni mechi ya ushindani mkubwa, si rahisi mchezo dhidi ya Yanga ilikuwa ni moja ya maandalizi yetu kuelekea mechi hiyo ya michuano ya kimataifa ambayo tunatarajia kucheza hivi karibuni," alisema Gomes.

Alisema wanatarajia kuondoka nchini leo kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mechi hiyo.

"Tunaanzia ugenini, ni mchezo muhimu, wachezaji wanajua umuhimu wa mchezo huo hivyo tunahitaji kwenda kutafuta matokeo chanya ili kuendelea kujiimarisha kwenye safari yetu ya Ligi ya Mabingwa Afrika," alisema Gomes.

Imeandikwa na Saada Akida na Adam Fungamwango

Chanzo: ippmedia.com