Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes Aifanyia Umafia Yanga

Simbasctanzania 240512249 384745193012865 3817581824395065233 N?fit=1080%2C719&ssl=1 Gomes Aifanyia Umafia Yanga

Sun, 12 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

GKUELEKEA mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga utakaopigwa Septemba 25, mwaka huu, Benchi la Ufundi la Simba chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes, limepanga kufanya umafia kuwasoma wapinzani wao hao.

Simba wamesema kwamba, kabla ya kukutana na Yanga, wataichunguza timu hiyo namna ya inavyocheza sambamba na ubora wa kikosi chao kwenye mechi zao mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika itakapocheza dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Chanzo chetu kutoka ndani ya Simba, kimeliambia Spoti Xtra kuwa: “Tumewaona Yanga katika mchezo uliopita dhidi ya Zanaco, lakini kwa kuwa mchezo ule haukuwa wa kimashindano, sasa benchi la ufundi chini ya Kocha Gomes linajiandaa kuwachunguza zaidi wapinzani wetu hao katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ili kujua ubora na mapungufu waliyonayo kwa ajili ya kuhakikisha tunawafunga.”

Chanzo: globalpublishers.co.tz