Emmanuel Giniki ametwaaa ubingwa wa nusu marathoni (kilomita 21) kwenye mbio ya Mbeya Tulia Marathoni (MTM) huku Failuna Abdi nyota wa timu ya taifa akikwaa kisiki kwa wanawake.
Mbio hiyo inayofanyika kwa siku ya pili imeongozwa na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ambaye alikimbia na kumaliza zile za kilomita tano wakiwa na wakimbiaji mbalimbali.
Kwenye nusu marathoni, Giniki aliibuka kidedea akitumia saa1:03:52 akiwapiku nyota wengine wa Tanzania na wanariadha wengine kutoka Kenya.
Joseph Panga alimaliza wa pili akikimbia kwa saa 1:04:15 na Mkenya, Kipruto akihitimisha tatu bora akitumia saa 1:06:15.
Bingwa wa zamani wa dunia, Fabiano Joseph alimaliza wa nane.
Upande wa wanawake, Marcelina Mbua aliibuka kinara akiwapiku nyota wa timu ya taifa, Jackline Sakilu na Failuna Abdi ambao walimaliza wa tatu na wanne huku Magdalena Shauri akimaliza wa pili.
Mbio ya kilomita 42, mpaka saa 8:45 ilikuwa inaendelea ambapo kwa wanawake, Sarah Ramadhan alikuwa akichuana na Wakenya wawili kwenye kundi la kwanza.