Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Giniki afuzu kushiriki mbio za dunia

Ginik Pic Data Giniki afuzu kushiriki mbio za dunia

Sun, 15 May 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mwanariadha wa Kimataifa wa Tanzania, Emanuel Giniki Gisamoda amefanikiwa kufanya kweli huko nchini Uswis baada ya kushinda mbio za Generali Geneve marathon zilizomalika leo.

Giniki amefanikiwa kukata utepe wa ushindi katika mbio hizo za kilomita 42, akitumia saa 2:10:39, na kuwapita wanariadha wa Kenya Sila Kiptoo aliyemaliza nafasi ya pili akitumia saa 2:11:31 na Stanley Bett aliyemaliza katika nafasi ya tatu kwa saa 2:12:01.

Ushindi wa Giniki katika mbio hizo, umemfanikisha rasmi kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia yatakayofanyika Oregon Marekani Julai 15 Mwaka huu.

Kocha wa Giniki, mwanariadha wa zamani, Alfredo Shahanga amesema kuwa amefurahia sana ushindi wa mwanafunzi wake huku akiahidi kumpa mazoezi mazuri zaidi.

"Nimefurahia Sana Giniki kushinda hasa alipopata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya dunia, na sasa najua nimepata kibarua cha ziada kuhakikisha anapata mafunzo mazuri zaidi kufanikisha kufanya vema mashindano ya dunia". amesema kocha Shahanga.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz