Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Giggs alia na Man United ilivyowachukulia poa Jesus na Mbappe

551 47772B8800000578 5205089 Image A 6 1513931849109 TZW

Sat, 23 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Uongozi wa klabu ya soka Manchester United unaweza ukawa unavumilia maumivu makali yanayochoma ndani ya mioyo yao baada ya kupuuzia kuwasajili wachezaji ambao ni hatari kwa sasa katika ufungaji wa mabao.

Hii inaweza ikawa kama ndoto lakini tayrai imeshatokea. Unaweza kuamini uongozi wa timu hiyo ulikataa kusikiliza mawazo ya Ryan Giggs kwa ajili ya kuwasajili Gabriel Jesus na Kylian Mbappe kipindi ambacho hata hawafahamiki katika soka.

Akiongea na The Times, Giggs ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi katika msimu wa 2014/16, amesema katika wakati huo wachezaji hao walikuwa wanapatikana kwa kiasi cha pauni million 5 tofauti na thamani yao ilivyokuwa kwa sasa.

“I watched Gabriel Jesus play three years ago,’ Giggs told The Times. ‘I watched Mbappe for a year. I was watching them with the scout and it was a no-brainer. It was just like. Get them. It would have been £5million or something — get them, loan them back — and that’s where the recruitment could have been better,” amesema Giggs.

Chanzo: bongo5.com