Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gekul aipongeza Simba Queens

Simba Queens Pic Data Gekul aipongeza Simba Queens

Mon, 17 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dodoma. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul ameipongeza timu ya soka ya wanawake ya Simba Queens  kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women Premier League) 2020/21.

Gekul akizungumza jijini Dodoma leo Jumatatu Mei 17 wakati timu hiyo ilipotembelea Bungeni amesema Simba Queens imestahili kushinda ubingwa huo kutokana na namna ilivyokuwa inapambana uwanjani kwenye michezo yake.

"Nina wapongeza viongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wote kwa juhudi kubwa mlizoonyesha katika kipindi chote cha ligi na kuweza kuwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo," amesema Gekul.

"Ligi ilikuwa na ushindani mkubwa lakini mmeweza kuibuka washindi, hii ni ishara kuwa ligi yetu ya wanawake inazidi kuimarika,"  amesema Gekul.

Timu ya Simba Queens imepata mwaliko maalumu wa kutembelea bungeni leo tarehe 17 Mei, 2021 mara baada ya kutwaa taji la ligi ya wanawake kwa kuifunga timu ya Baobab Queens bao1-0 katika mchezo uliofanyika jana kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz