Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geay mzigoni Boston Marathon kesho

Gabriel Geay Geay mzigoni Boston Marathon kesho

Sun, 14 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania, Gabriel Geay ameweka wazi amejiandaa kushinda mbio za Boston Marathon zitakazofanyika kesho Aprili 15.

Ikumbukwe mwaka 2023, Geay alimaliza wa pili katika mbio hizo kongwe za Dunia za 127 za Boston, Marekani kwa kumaliza kilomita 42 kwa saa 2:06.06 nyuma ya Mkenya Evans Chebet aliyeongoza kwa 2:06:04.

Kupitia mbio hizo, Geay aliwashangaza wengi baada ya kumpiku mkongwe na ambaye amekuwa akishikilia rekodi mbalimbali za Dunia katika riadha, Eliud Kipchoge kutoka Kenya tukio ambalo ni nadra sana kwa mwanariadha wa Tanzania.

Geay ambaye anashikilia rekodi ya taifa kwa kumaliza mbio ndefu akitumia muda wa saa 02:04 akiongea na Mwanaspoti amesema amejiandaa vizuri kupambana kufanya vyema.

“Natarajia nitakimbia viuri japo siwezi kusema nitashinda kwani sijui wapinzani wangu wamejiandaa vipi, lakini nimefanya maandalizi ya kutosha,” amesema Geay.

Mwanariadha huyo ambaye alimaliza wa saba katika mashindano ya dunia mwaka 2022 ameongeza kama mambo yataenda vizuri jinsi ambavyo amepanga anaamini kesho ataipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa kwa kuongoza na kuwashinda wababe wa mbio hizo kwa dunia.

“Natambua kutakuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wanariadha wengine, ndiyo maana nimejitahidi kufanya maandalizi ambayo yatanifanya kwenda kushinda kesho,” amesema Geay.

Mwanariadha huyo ambaye alianza na mbio ndefu za viwanjani (mita 5000 na 10000) amesema baada ya kumaliza Boston Marathon akili na nguvu zote ataelekeza katika Marathoni za Olimpiki zitakazofanyika Paris Ufaransa, Julai mwaka huu.

Chanzo: Mwanaspoti