Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gadiel awaangukia Watanzania

69067 Gardi+pic

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

BEKI wa Taifa Stars, Gadiel Michael amewaomba Watanzania kuwaunga mkono kuelekea mechi yao ya marudiano na Kenya ya michuano ya wachezaji wa ndani Afrika (CHAN), akidai wanawaza ushindi na sio kushindwa.

Gadiel anasema anatambua Watanzania wengi walikuwa wana matumaini makubwa ya Stars kushinda Uwanja wa Taifa, lakini ikaja sivyo ndivyo jambo alilowaambia lisiwavunje moyo.

Stars itakwenda kurudiana na Kenya, Agosti 4, jambo ambalo Gadiel linampa kujiamini kwamba wana uwezo wa kwenda kushinda ugenini bila kujali walichokivuna taifa.

"Watanzania wanapaswa kutambua kwamba hakuna mchezaji duniani ambaye anapenda kufungwa na kwamba kusuluhu taifa hata wao ni kitendo kilichowaumiza na kinawaongezea umakini wa kwenda kupambana zaidiĀ  ugenini.

"Michuano hii ni faida kwetu wachezaji kuonyeshana uwezo na kwamba licha ya kwamba hatucheza nje tuna uwezo wa kufanya kitu cha tofautiĀ  na ndio maana naendelea kusisitiza kwamba matokeo yalituumiza sisi ni Watanzania tunahitaji bendera yetu ipepe vyema dhidi ya wapinzani wetu,"anasema.

***

Chanzo: mwananchi.co.tz