Sir Frank Williams, mwanzilishi na mkuu wa zamani wa timu ya Williams Racing, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.
Williams aliichukua timu yake ya mbio za magari kutoka sifuri hadi kwenye kilele cha Formula One, akisimamia ushindi mara 114, mashindano 16 ya ulimwengu ya madereva, huku akiwa bosi wa timu aliyekaa muda mrefu zaidi katika historia ya mchezo huo.
“Baada ya kulazwa hospitalini siku ya Ijumaa, Sir Frank aliaga dunia asubuhi ya leo akiwa amezungukwa na familia yake,” Timu ya Williams Racing ilisema katika taarifa siku ya Jumapili.
Maisha ya Williams ni ya ajabu zaidi kutokana na ajali mbaya ya gari aliyoipata nchini Ufaransa iliyomsababishia majeraha makubwa hivyo madaktari walifikiria kuzima mashine yake ya kusaidia maisha.
Lakini mke wake Virginia aliamuru kwamba mumewe abakishwe hai na azimio lake kamili na ujasiri – sifa ambazo zilifananisha kazi yake – zilimwezesha kuendelea na mapenzi ya maisha yake.
Alisalia katika nafasi yake ya mkuu wa Williams Racing kwa miaka 34 zaidi kabla ya familia hiyo ya Formula 1 kuiuza kwa mwekezaji wa Marekani mwezi Agosti.