Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fiston Atuma Salamu Yanga, Asajiliwa Morocco

FISTON.png?fit=781%2C430&ssl=1 Fiston Atuma Salamu Yanga, Asajiliwa Morocco

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Fiston Abdulrazack, ametuma salamu za kuwaaga wana Yanga baada ya kusajiliwa na Olympique Club ya Morocco kwa mkataba wa miaka miwili.

Siku chache zilizopita wakati Simba walipoweka kambi Morocco, walicheza mchezo wa kirafiki na klabu hiyo na kutoka sare ya bao 1-1.

Timu hiyo inatajwa kuwa kongwe sana nchini humo.Kwa muda wa miezi sita ambao Fiston aliitumikia Yanga, alifanikiwa kufunga mabao matatu.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Fiston amesema: “Nawashukuru wana Yanga kwa muda wao na sapoti waliyonionyesha kwa miezi sita, kwa sasa nipo Morocco kwenye timu yangu mpya.“Nimesaini mkataba wa miaka miwili na nina imani nitakuwa na wakati mzuri nikiwa hapa.”

Chanzo: globalpublishers.co.tz