Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fiston Afungasha Kila Kitu, Asepa Yanga

FISTON.png?fit=708%2C398&ssl=1 Fiston Afungasha Kila Kitu, Asepa Yanga - Global Publishers

Tue, 13 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Fiston Afungasha Kila Kitu, Asepa Yanga July 13, 2021 by Global Publishers



MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Abdoul Razack, amefungasha kila kitu kilicho chake, kisha kutimka kambini, huku akijiandaa kutimkia kwao Burundi.

Mrundi huyo ambaye alisaini kandarasi ya miezi sita kuichezea Yanga, mkataba wake huo umemalizika rasmi jana Jumatatu, hivyo akachukua uamuzi huo haraka sana.

Tangu ajiunge na Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu, Fiston amefunga mabao mawili katika michuano yote ambapo moja Ligi Kuu Bara na lingine Kombe la FA.

Akizungumza na Spoti Xtra, Fiston amesema kuwa: “Nilimwambia injinia (Hersi Said) kuwa Julai 12 mkataba wangu unaisha, hivyo naondoka, nilimwambia hivyo usiku ule tulipokuwa tunapata chakula cha usiku (Jumamosi iliyopita).

“Alinisisitiza kubaki mpaka mwisho wa msimu kwa sababu ligi imechelewa kuisha, ila nikakataa, naona bora nirudi nyumbani maana mkataba wangu umeisha.“

Hivyo leo (jana) nimechukua kila kilicho changu, nimeondoka kambini na kurudi nyumbani. Hivi karibuni natarajia kwenda kusalimia wazazi nyumbani Burundi.”

Stori: Careen Oscar, Dar

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz