Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto aharibu, atetewa

49350 Fei+pic

Fri, 29 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MASHABIKI wa Yanga huwa wanapata mazuka wanapomuona kiungo wao fundi, Feisal Salum ‘Fei Toto’ akiwa ameshika mpira uwanjani.

Hiyo inatokana na uwezo wake wa kuchezea mpira na kupiga pasi zenye macho uwanjani, lakini habari hizi zinaweza kuwashtua na wakabisha hadi asubuhi.

Mwanaspoti limechimbua katika rekodi na taarifa mbalimbali za Ligi Kuu Bara msimu huu na kubaini kwamba, Fei Toto ndiye mchezaji mwenye kadi nyingi za njano huku wanaomfutia wakiwa na kadi nane na saba.

Fei Toto alijiunga na Yanga msimu huu akitokea JKU ya Zanzibar na katika usajili wake ulizua gumzo, baada ya kubaini alisaini mkataba na Singida na Simba pia walikuwa wanasaka saini yake.

Kadi za Fei Toto zilitokana na mechi za Stand United, Singida United, Mbao, Kagera Sugar, JKT Tanzania, Tanzania Prisons, Ruvu Shooting, Singida United na Simba.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera, amemkingia kifua kiungo wake huyo kuwa na idadi kubwa ya kadi za njano ni kutokana na kucheza michezo mingi mfululizo huku akikamiwa na wachezaji wa timu pinzani.

Alisema Fei Toto ni moja ya wachezaji wenye nidhamu ya mchezo na kukutwa na idadi kubwa ya kadi ni kutokana aina ya uchezaji wa timu ambazo zinaikamia sana Yanga.

“Tuna ratiba ngumu sana tumekuwa tukicheza mfululizo na tunapata matokeo hivyo timu nyingi zinaingia uwanjani kwa kutukamia na hiyo ndio sababu ya kadi za Fei Toto,” alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz