Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto: Msiogope, hii ni Yanga mpya kabisa

Fei Pic Data Fei Toto: Msiogope, hii ni Yanga mpya kabisa

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KIUNGO fundi wa Yanga na Taifa Stars, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kutokana na kukosekana kwa nyota watatu kwenye mchezo wa Jumapili na kusisitiza kuwa watapiga mzigo kwelikweli.

Staa huyo aliyefunga bao la ushindi kwa Taifa Stars dhidi ya Madagascar waliposhinda mabao 3-2 juzi Jijini Dar es Salaam, alisema Yanga ya sasa sio ile ya misimu iliyopita.

Yanga itawakosa Khalid Aucho, Djuma Shaban na Fiston Mayele kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United.

Akizungumza na Mwanaspoti, Fei Toto alisema: “Tuna timu nzuri na wachezaji wenye uzoefu hivyo kuondoka kwa wachezaji watatu ambao pia ni wapya kikosini kusiwape hofu mashabiki wetu wanatakiwa kuwaamini nyota wote waliosajiliwa ni bora na wanajitambua.

“Tunaanza kucheza uwanja wa nyumbani tunahitaji kuonyesha kwa kupata matokeo mazuri hili linawezekana kwa kufanya kile tunachoelekezwa na mwalimu na kuongeza uwezo wa mchezaji mmoja mmoja,” alisema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz