Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia yaishi ndani ya shimo miaka tisa

80494 Familia+pic

Thu, 17 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Uholanzi. Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni, ndivyo unavyoweza kusema baada ya polisi nchini Uholanzi kugundua chumba cha siri cha chini ya ardhi kilichokuwa kikitumika na familia moja kwa zaidi ya miaka tisa.

Taarifa ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari ilisema kuwa chumba hicho kimegunduliwa na kuacha maswali mengi yasiyo na majibu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, familia hiyo ilikuwa ikiishi chini ya ardhi kwa kile walichodai kuwa ilikuwa ikisubiri siku ya ‘mwisho wa dunia’.

Shirika la Utangazaji la BBC, liliandika kuwa mwanaume wa miaka 58 na watoto wake sita walio na umri kati ya miaka 16 hadi 25 walikuwa wakiishi katika chumba hicho kilichopo katika shamba lao lililopo Mkoa wa Kaskazini wa Drenthe.

“Walipatikana baada ya kijana wake mkubwa kwenda kununua pombe katika baa moja karibu na kijiji cha Ruinerwold na kumfahamisha mhudumu wa kwamba anataka usaidizi,” kituo cha Televisheni cha RTV kiliripoti.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa muhudumu huyo alimuona kijana huyo kama amechanganyikiwa na kupuuza ombi hilo mpaka pale alipotokea mwanakijiji mwingine na kumsikiliza kwa umakini.

Pia Soma

Advertisement
“Aliagiza chupa tano za bia na kunywa zote. Baada ya hapo nilizungumza nae kidogo ndipo alipofichua kuwa ametoroka na kwamba anaomba usaidizi... tukapiga simu polisi,” mmiliki wa baa hiyo Chris Westerbeek alikifahamisha kituo cha RTV.

Aliongeza kuwa, “alikuwa na nywele ndefu, kucha ndevu chafu, nguo zilizochakaa na alionekana kana kwamba amechanganyikiwa. Alisema hajawahi kwenda shule na kunyolewa nywele kwa miaka tisa.

“Alisema ana ndugu na dada zake ambao wanaishi katika shamba hilo. Pia, alisema anataka kukomesha jinsi familia yake inavyoishi.”

Wakizungumza na waandishi wa habari majirani wa familia hiyo walisema wanaamini watu hao walikuwa wakiishi kwa kula mboga za majani pekee ambazo zimepandwa katika shamba hilo.

Maofisa wa polisi waliootembelea makazi hayo ili kufanya upekuzi zaidi waligundua ngazi iliyokuwa nyuma ya kabati katika sebule ya nyumba hiyo ambayo inaelekea chumba hicho chini ya ardhi ambako familia hiyo ilikuwa ikiishi.

Ruinerwold ni kijiji kilicho na wakazi chini ya 3,000. Shamba hilo lipo nje kidogo ya kijiji hicho ana inaweza kufikiwa tu kupitia daraja lililoko juu ya mfereji.

Shamba hilo ambalo kwa upande mmoja limefichwa na miti mingi pia limepandwa mboga nyingi.

Jirani mwingine aliviambia vyombo vya habari vya Uholanzi kuwa alimuona mtu huyo peke yake na alifikiri hana watoto.

Chanzo: mwananchi.co.tz