Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia ya mwanariadha wa Rwanda aliyeuawa Kenya yatoa wito wa "ukweli na haki"

Familia Ya Mwanariadha Wa Rwanda Aliyeuawa Kenya Yatoa Wito Wa Familia ya mwanariadha wa Rwanda aliyeuawa Kenya yatoa wito wa "ukweli na haki"

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Familia ya mwanariadha wa Rwanda aliyeuawa katika mji maarufu wa magharibi mwa Kenya inatoa wito wa "ukweli na haki" kwa mtoto wao ambaye "alikuwa akifuatilia shauku yake ya kukimbia na kuwa bora kichezo".

Polisi inasema inachunguza tukio hilo lililosababisha kifo cha Siragi Rubayitaambacho vyombo vya habari vya eneo hilo vilikihusishwa na suala la "mzozo wa mapenzi " katiya Bw Rubayita, na wanariadha wawili wa Kenya wa kike na kiume ambao kwa sasa ni washukiwa wakuu wa kifo hicho.

Bw Rubayita, 34, mwanariadha wa masafa marefu ambaye alikuwa akifanya mazoezi katika eneo la Iten, Kaunti ya Elgeyo Marakwet,kabla ya mashindano nchini Italia, aliuawa katika "kitendo kisicho na maana cha vurugu... wakati mwanariadha mwenzake na mpenzi wake walipomwalika nyumbani kwao usiku kabla ya kuondoka kwake," familia yake ilisema katika taarifa.

Nasra Bishumba,dada wa Bw Rubayita, aliiambia BBC kwamba kaka yake alitarajiwa kurudi nyumbani Kigali siku yaIjumaa kabla ya kuondoka kwenda Italia.

Alisema wakufunzi wakee huko Iten walikuwa "wamejitosa katika kumtafuta wakati mwanariadha waliyelala naye chumba kimoja alipotoa tahadhari kuwa hajarejea kulala.

"Baada ya kutuarifu, mara moja walianza kufanya kazi na polisi na hivyo ndivyo watuhumiwa walivyokamatwa."

Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kuwa mwanariadha wa kiume wa Kenya hakufurahishwa na uhusiano kati ya mwanariadha huyo wa Rwanda na mwanariadha wa kike wa Kenya.

Uchunguzi wa mwili wa Bw Rubayita unatarajiwa kufanyika, nafamilia yake imetuma ujumbe wake Iten"kumrudisha nyumbani ambako tunatarajia kumpa upendo na kumuenzi kulingana na alivyokuwa mtoto na kaka wa kipekee ", dada yake ameiambia BBC.

Ubalozi wa Rwanda nchini Kenya umeiambia BBC katika taarifa yake kwamba "mwanadiplomasia kutoka ubalozi huo yuko tayari kufuatilia kesi hiyo".

Rubayita ameiwakilisha Rwanda katika mashindano ya kimataifa barani Afrika na Ulaya, mwezi Juni alikimbia mbio za nusu marathon kwa muda wa saa 1:05:34 katika mbio za mji wa Kigali -Kigali International Peace Marathon akichukua nafasi ya 13.

Chanzo: Bbc