Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia ya Schumacher yashinda kesi dhidi ya Mwandishi wa Ujerumani

Skynews Michael Schumacher 6563753 Michael Schumacher

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia ya Dereva maarufu wa Magari ya Formula 1 Michael Schumacher, imeshinda kesi dhidi ya mchapishaji wa Gazeti aliyechapisha mahojiano yaliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili janja ( Articifical intelligence).

Schumacher (55), aliyepata ajali mbaya mwaka 2013 wakati akicheza kwenye theluji, anaishi nyumbani na familia yake nchini Uswizi.

Dereva huyo ambaye ni Bingwa mara 7 wa Mashindano ya magari ya Formula 1 hajaonekana hadharani kwa zaidi ya miaka 10, na hajawahi kuzungumza na chombo chochote cha habari.

Vilevile familia yake imeamua kuwa na faragha na hivyo imekaa kimya kabisa kuhusu maendeleo ya hali yake.

Mnamo Aprilli 2023, Gazeti la Die Aktuelle la Ujerumani lilichapisha mahojiano ambayo lilidai kuwa ni maneno ya Schumacher.

Katika ukurasa wa mbele kabisa, gazeti hilo liliandika kichwa cha habari kilichosema “ Mahojiano ya kwanza na Michael Schumacher”

Funke Media Group ambao ndio wachapishaji wa gazeti hilo waliiomba familia msamaha na walimfukuza kazi Mhariri aliyehusika na habari hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live