Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Failuna hoi Karatu

Fai Pic Data Mwanariadha Failuna Abdi ameshindwa kung'ara Karatu

Fri, 24 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanariadha nyota wa mbio ndefu nchini, Failuna Abdi ameshindwa kutamba na kumaliza wa saba kwenye mbio za kilomita tano katika tamasha la Karatu linaloendelea kwenye uwanja wa Mazingira Bora mjini hapa.

Failuna aliyetumia dakika 20:30:03 aliachwa kwa zaidi ya dakika 1:30 na bingwa mpya wa mbio hiyo, Natalia Elisante aliyetumia dakika 18:34:20.

Hadi mzunguko wa kwanza unamalizika, Failuna bingwa wa msimu uliopita alikuwa akiongoza, kabla ya kuanza kupitwa akiwa amebakiza kilomita 2 kumaliza mbio hiyo na kumaliza wa saba.

Baada ya kumaliza mbio hiyo, Failuna alilazimika kupewa huduma ya kwanza kufuatia kuishiwa nguvu tofauti na washiriki wengine.

Nyota wengine waliochuana ni Mayselina Mbua aliyemaliza wa pili akitumia dakika 18:51:28, Annastazia Dolomongo aliyetumia dakika 19:30:83 na kuwa watatu.

Wengine waliomfunika Failuna ni Asha Salum, Aisha Lubuma na Sarah Ramadhan.

Mbio ya Karatu inayodhaminiwa na Olympic Solidarity (OS) kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) ni tano kwa Failuna kukimbia ndani ya miezi mitatu ikiwamo moja ya kimataifa aliyokimbia hivi karibuni nchini Hispania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live