Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA yabariki kifungo cha Wambura

38220 Wambura+pic FIFA yabariki kifungo cha Wambura

Fri, 25 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa), imemfungia maisha, Michael Wambura kujishughulisha na masuala yanayohusiana na soka.

Katika uamuzi wake uliotolewa Januari 22, 2019 na kutumwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kamati hiyo iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Anin Yeboah wa Ghana, imekazia hukumu ya Kamati ya Rufani ya Maadili ya TFF iliyotolewa Aprili 6, 2018.

Baada ya kamati hiyo kukazia rufani hiyo, Wambura ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa TFF hatakiwi kujishughulisha na masuala ya soka duniani kote.

Taarifa ya TFF ilisema Fifa imemkabidhi Wambura uamuzi huo na imewataka wadau wa soka kuzingatia maadili na nidhamu kwa kufuata utaratibu kwa mujibu wa Katiba za TFF, CAF na Fifa.

Wambura alifungiwa na kamati ya maadili kwa makosa matatu kwa madai ya kuchukua fedha za malipo ya TFF ambayo hayakuwa halali na kinyume na kifungu cha 73 (1) cha kanuni za maadili za TFF toleo la 2013.

Pia alituhumiwa kughushi barua ya kuelekeza alipwe malipo ya kampuni ya Jekc Systems Limited huku akijua malipo hayo si halali ni kinyume na kifungu cha 73 (7) cha kanuni za maadili ya TFF toleo la 2013.

Kamati hiyo ilida vitendo hivyo vilishusha hadhi ya shirikisho hilo ikiwa ni kinyume na ibara ya 50 (1) ya Katiba ya TFF kama ilivyorekebishwa 2015.

Hata hivyo, Wambura alirudishwa madarakani baada ya Mahakama Kuu kutengua hukumu hiyo na kuamuru kurejea katika wadhifa wake kabla ya TFF kwenda Fifa. Kabla ya kushika wadhifa wa Makamu wa Rais, Wambura aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa TFF (zamani FAT).



Chanzo: mwananchi.co.tz