Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIA Yamvua Ukurugenzi Masi wa F1

FIA FIA Yamvua Ukurugenzi Masi wa F1

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

FIA yathibitisha kumuondoa Michael Masi kwenye nafasi ya ukurugenzi wa mashindano ya Formula 1 kufuatia uchunguzi uliofanyika wakati akisimamia mashindano ya Abu Dhabi Grand Prix.

Kuanzia sasa nafasi ya ukurugenzi wa mashindano itakuwa inasimamiwa na mkurugenzi wa World Endurance Championship Eduardo Freitas, akishirikiana na mkurugenzi wa mbio za DTM Niels Wittich.

Raisi wa FIA Mohammed Ben Sulayem kutokana na video iliyotolewa na shirikisho hilo kwenye mbio za Abu Dhabi Grand Prix, wametangaza kufanya mabadiliko ya jinsi ya kuziendesha mbio hizo, kwa kuanzisha “virtual race control” (VAR), Sulayem alipokuwa jijini Uingereza alinukuliwa akisema,

“Awali ningependa kutangaza kuwa kunaunzishwaji mpya wa wa chumba cha “virtual race control” ni kama mwamumzi msaidizi amayetumia video kwenye mpira, pili mawasiliano ya radio wakati wa mbio, kwa sasa yalikuwa yanaonyeshwa moja kwa moja, yataondolewa ili kumlinda mkurugenzi kutokaa na presha za nje.

Mwisho ningependa kutangaza uongozi mpya ambao utanza kazi jijini barcelona kwa majaribio ya msimu, Niels Wittich na Eduardo Freitas watakuwa wakurugenzi wa mashindano, wakisaidiwa na Herbie Blash kama mshauri wa kudumu, Michael Masi, atapangiwa kazi nyingine.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live