Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FA CUP YATARAJIWA KUTIMUA VUMBI RASMI APRILI 7,2021

JP 1.png?fit=468%2C258 FA CUP YATARAJIWA KUTIMUA VUMBI RASMI APRILI 7,2021

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Hatua ya 16 bora ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Zanzibar (FA CUP) inatarajiwa kuanza kutimua Vumbi lake mapema Aprili 7 mwaka huu ambapo Bingwa wa Mashindano hayo ataiwakilisha Zanzibar katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Africa CAF.

Timu zilizofanikiwa kutinga hatua hiyo ya 16 kwa upande wa Unguja ni Black Sailor , Mchangani United3, New King, Taifa Jang’ombe, .Chuoni FC, Umoja Mbuzini, Dulla boys, .JKU, Kundemba, Mlandege, .Wembe, KMKM, Polisi, M/ Makumbi City, Zimamoto, Kilimani City.

Bingwa wa Michuano hiyo kwa Kanda ya Unguja atacheza na Bingwa wa Kanda ya Pemba Ili kupata timu itakayoiwakilisha Zanzibar katika michuano hiyo ya CAF, hata hivyo Kanda ya Pemba bado michuano hiyo haijaanza kutokana na mgomo uliopo wa timu za Ligi daraja la kwanza Kanda ya Pemba

Chanzo: zanzibar24.co.tz