Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

F1: Kibarua cha Masi Shakani Baada ya Uchungzi wa FIA

Max Kibarua cha Masi Shakani Baada ya Uchungzi wa FIA

Wed, 16 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya sintofahamu kwenye fainali ya Formula 1 mwaka 2021 ambapo Max Verstappen kuibuka na ushindi kwenye mashindano hayo akimzidi mbabe huyo wa F1 Lewis Hamilton FIA ilianza uchunguzi kufuatia malalamiko ya timu ya Mercedes.

FIA iliwasilisha matokeo ya uchunguzi wao kuhusu mwisho wa msimu wa 2021 wa Formula 1 siku ya Jumatatu, huku kukiwa na uvumi kuhusu mustakabali wa mkurugenzi wa mbio Michael Masi.

Nafasi ya Masi ipo shakani na uenda akondlewa kwenye nafasi hiyo baada ya uamuzi wake wa kuanzisha tena mbio Abu Dhabi GP, ambayo ilitoa fursa kwa Max Verstappen kumpita Lewis Hamilton na kushinda taji kwenye mzunguko wa mwisho wa mbio.

Mashabiki walikasirishwa na walidai Hamilton alinyang’anywa taji, hali iliyopelekea FIA kufanya uchunguzi kuhusu mzunguko wa mwisho wa Grand Prix.

Endapo FIA itaamua kufanya mabadiliko yoyote, yatahitaji kuidhinishwa na Baraza la Michezo la Michezo ya Magari mwezi Machi 18, siku mbili tu kabla ya GP ya ufunguzi wa msimu wa Bahrain.

Hiyo inamaanisha kuwa matokeo ya FIA hayatawekwa wazi siku mbili tu kabla ya kuanza kwa msimu wa 2022 F1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live