Mwanariadha kutoka Kenya, Eliud Kipchoge (38) ameshinda marathon yake ya tano huko Berlin (Ujerumani) asubuhi ya jana Jumapili, kwa muda wa saa 2:02:42.
Kipchoge anakuwa mshindi wa mara nyingi zaidi katika marathon ya Berlin ( #berlinmarathon ) na ushindi wake wa tano, kufuatia ushindi wake miaka ya 2015, 2017, 2018, 2022, na sasa 2023.
Huku Mwanadada Tigist Assefa (29) kutoka ethiopia amevunja rekodi upande wa wanawake. Assefa, ambaye pia alishinda mbio za mwaka jana, alimaliza kwa muda wa saa 2, dakika 11, na sekunde 53.
Mwanadada Asefa alipunguza zaidi ya dakika mbili kutoka kwa rekodi ya awali ya saa 2:14.04 - iliyowekwa na Mkenya Brigid Kosgei huko Chicago mwaka 2019.
Orodha kamili ya Washindani hii hapa
1. Eliud Kipchoge (KEN) -- 2:02:42
2. Vincent Kipkemoi (KEN) -- 2:03:13
3. Tadese Takele (ETH) -- 2:03:24
4. Ronald Korir (KEN) -- 2:04:22
5. Haftu Teklu (ETH) -- 2:04:42
6. Andualem Shiferaw (ETH) -- 2:04:44
7. Amos Kipruto (KEN) -- 2:04:49
8. Philemon Kiplimo (KEN) -- 2:04:56
9. Amanal Petros (GER) -- 2:04:58
10. Bonface Kimutai Kiplimo (KEN) -- 2:05:05